Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 70 wafariki baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka Mali

Kuporomoka Mali Watu 70 wafariki baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka Mali

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachimba migodi wasiopungua 70 wamefariki dunia baada ya kuporomokewa na udongo kwenye barabara ya chini kwa chini ya kuingia kwenye mgodi wa dhahabu kusini magharibi mwa Mali.

Hayo yalisemwa jana Jumatano na Karim Berthe, afisa katika Idara ya Taifa ya Jioljia na Madini ya Mali katika kikao na waandishi wa habari huko Bamako, mji mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Berthe amebainisha kuwa, ajali hiyo ilitokea Ijumaa iliyopita katika mji wa Kobadani mkoa wa kusini magharibi wa Kolikouro na kuongeza kuwa, uchunguzi wa kubaini chanzo cha mkasa huo umeanza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Anadolu, timbo hilo lilikuwa na wachimba migodi 200 wakati wa ajali hiyo. Awali Wizara ya Madini ya Mali ilitoa taarifa na kusema kuwa, watu kadhaa wamepoteza maisha katika ajali hiyo.

Mali ni mzalishaji mkubwa wa tatu wa dhahabu barani Afrika, huku madini hayo yakichangia asilimia 25 ya bajeti ya taifa. Hata hivyo shughuli za uchimbaji madini katika aghalabu ya matimbo ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika zinafanyika kinyume cha sheria na bila ya uangalizi wa vyombo vya dola.

Takwimu zinaonyesha kuwa, aghalabu ya madini hususan ya dhahabu yanayochimbwa kinyume cha sheria nchini humo pamoja na nchi nyingine za Afrika, husafirishwa kimagendo katika nchi za Ulaya na Uarabuni.

Katika hatua nyingine, serikali ya Kenya imetangaza kuwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki imegundua kuwa na akiba kubwa ya madini ya coltan katika kaunti ya Kiambu, mashariki mwa nchi.

Waziri wa Madini na Uchumi wa Buluu wa Kenya, Salim Mvurya alisema hayo jana Jumatano na kuongeza kuwa, madini hayo yanayotumika katika uzalishaji wa simu za rununu na laptopu (vipakatakilishi) yamegunduliwa katika kaunti sita za nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live