Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 60 wafariki katika moto uliozuka mjini Johannesburg

Watu 60 Wafariki Katika Moto Uliozuka Mjini Johannesburg Watu 60 wafariki katika moto uliozuka mjini Johannesburg

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: Voa

Takriban watu 63 wamefariki baada ya moto kuzuka katika jengo moja mjini Johannesburg, mamlaka ya Afrika Kusini inasema.

Wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa. Maafisa wa Johannesburg wanasema haijafahamika ni nini kilisababisha moto huo katika jengo la ghorofa tano katikati mwa jiji.

Msemaji wa huduma za dharura, Robert Mulaudzi, aliambia BBC kwamba wazima moto wameweza kuwatoa baadhi ya watu waliokuwa ndani.Alisema moto huo uliteketeza jengo hilo, na kwamba msako wa kuwatafuta waathiriwa wengine unaendelea."

Tunapanda ghorofa hadi ghorofa tukifanya shughuli za uokoaji wa miili hii," Bw Mulaudzi aliambia shirika la utangazaji la ENCA.

Video iliyotumwa kwa jukwaa X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter, na Bw Mulaudzi ilionyesha magari ya zimamoto na ambulensi nje ya jengo hilo na madirisha yaliyoteketea.

Picha kutoka eneo la tukio zilionyesha miili iliyofunikwa ikiwa imejipanga karibu na jengo lililoungua.

Ripoti zinaonyesha waliokuwa ndani ya jengo hilo walikuwa wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika.

Chanzo: Voa