Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 60 wafariki dunia baada ya boti kuzama nchini DRC Congo

0568d598f5d7bfc6094332c7d7836fa7 Watu 60 wafariki dunia baada ya boti kuzama nchini DRC Congo

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Takribani watu 60 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 100 wamepotea baada ya boti kuzama Mto Congo usiku wa kuamkia leo. Waziri wa Maswala ya Kibinadamu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amethibitisha.

Waziri Steve Mbikayi alisema zaidi ya watu 700 walikuwa ndani ya boti hiyo lakini hadi sasa watu 300 ndio wamepatikana eneo la janga katika mkoa wa Mai-Ndombe magharibi mwa nchi hiyo.

Waziri huyo alitaja chanzo cha boti hiyo kuzama kuwa ni migizo mingi na watu wengi waliozidi uwezo wa boti hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz