Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 6 wauawa, 10 wajeruhiwa katika shambulizi Somalia

Watu 6 Wauwawa, 10 Wajeruhiwa Katika Shambulizi Somalia Watu 6 wauawa, 10 wajeruhiwa katika shambulizi Somalia

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: Voa

Watu 6 wameuwawa na zaidi ya 10 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu kwenye gari Alhamisi katika jimbo la kati la Hirshabelle, Somalia, kwa mujibu wa maafisa.

Mshukiwa alilenga soko la nyama lenye shughuli nyingi katika mji wa Bulobarde, takriban kilomita 220 kaskazini mwa Mogadishu.

Saadaam Cabdi Iidow, meya wa mji huo, amesema mtu aliyejitoa muhanga alishaambuliwa na maafisa wa usalama kabla ya kufikia lengo japo alifanikiwa kulipua bomu kabla kufikia kizuizi cha polisi.

“Takriban watu sita wameuwawa na zaidi ya 10 wamejeruhiwa, wakiwemo watoto na wanajeshi wa kikosi cha usalama."

Mlipuko huo uliharibu eneo lote la biashara na baadhi ya majengo ya makazi,” Iidow alisema.

Wakati huo huo, maafisa wa usalama walizuia mashambulizi mawili ya mabomu ya kujitoa mhanga kwenye gari yaliyolenga Dhusamareb, mji ulioko umbali wa kilomita 280 kaskazini mwa Mogadishu.

Chanzo: Voa