Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 51 wamepokelewa nchini Uganda kutoka Afghanistan

Refugees Watu 51 wamepokelewa nchi Uganda kutoka Afghanistan

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuonesha utayari wa kuwapokea wahamiaji wanaohitaji hifadhi kutoka nchini Afghanistan, tayari serikali ya Uganda imekiri kupokea watu 51 ambao wamefika nchini humo kupata hifadhi ili kukwapa machafuko.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema watu hao wamewasili kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe August 24 asubuhi wakiwa kwenye ndege binafsi.

"Wamepitia taratibu zote za ukaguzi na vipimo ikiwemo COVID-19 na watakaa karantini kwa muda uliopangwa. Taarifa ya Wizara imefafanua.

Uganda imesema kuwa Marekani iliwaomba kupokea na kuwasaidia watu wanaohitaji hifadhi pamoja na wale wanaohitaji kuelekea nchini Marekani basi wanaweza kufikia nchini Uganda ili kujiondoa na hatari zinazoweza kutokea nchini Afghanistan.

Serikali imesema ilikubali ombi hilo la kuwapokea na kuwasaidia watu wanaokimbia machafuko ikiwa ni utaratibu wa utu wema na kufata makubaliano ya kimataifa linapotokea jambo kama hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live