Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 50 watekwa nyara na majambazi Cameroon

Ca,erron Watekwa Watu 50 watekwa nyara na majambazi Cameroon

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majambazi wenye silaha wamewateka nyara takriban watu 50 katika muda wa chini ya siku tatu zilizopita kwenye eneo la kaskazini mwa Cameroon.

Duru mbalimbali za habari zimetangaza habari hiyo na kusema jana Jumatano kwamba majambazi hao waliwavizia na kuwateka nyara watu wapatao 20 katika eneo la Touboro juzi Jumanne, ikiwa ni saa 48 tu baada ya kuwateka nyara wengine 30 katika eneo jingine moja la kaskazini mwa Cameroon.

Jumanne usiku, afisa mmoja wa usalama katika eneo hilo aliliambia shirika la habari la Xinhua kwamba msako unaendelea kugundua walikopelekwa mateka hao.

Vyombo vya habari vya kieneo vimeripoti kuwa, watu walianza kufungasha virago vyao na kutoroka katika eneo hilo ambalo limekuwa maarufu kwa vitendo vya utekaji nyara. Askari wa Cameroon wakiwa katika ulinzi

Tangu mwaka wa 2021, eneo la kaskazini mwa Cameroon, ambalo linashirikiana mpaka na nchi yenye migogoro ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, limekuwa kitovu cha vitendo vya utekaji nyara unaofanywa na majambazi wenye silaha. Wahanga wakubwa wa utekaji nyara huo wa mara kwa mara ni watoto na watu wanaosafiri kwenye barabara kuu. Vitendo vingi vya utekaji vinafanyika kwa shabaha ya kupata fedha za vikomboleo.

Vitendo vya utumiaji silaha vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara nchini Cameroon. Katikati ya mwezi Julai mwaka huu pia, watu wenye silaha waliua watu 10 na kuwajeruhi wengine wawili kwenye eneo moja lenye watu wengi katika mji wa Bamenda kaskazini magharibi mwa Cameroon kwa sababu hizo hizo za fedha.

Mbali na vitendo hivyo vya utekaji nyara, Camerooni inakabiliwa pia na mashambulizi ya magenge ya kigaidi kama vile Boko Haram ambalo linaendesha jinai zake nyingi, nchini Nigeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live