Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 50 Wauawa Katika Shambulio Niger

NIGER?fit=624%2C351&ssl=1 Watu 50 Wauawa Katika Shambulio Niger

Fri, 19 Mar 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Watu 58 wameuawa nchini Niger baada ya shambulio lililotokea katika mpaka wa Mali, mamlaka imeeleza. Wanaume wenye silaha walikuwa kwenye magari manne wakifyatua risasi karibu na soko katika eneo la Tillabéri.

Hakuna kundi la kigaidi lililodai kuhusika na shambulio hilo ambalo ilitokea Jumatatu. Hata hivyo hivi karibuni kulikuwa kampeni za jihadi wawili Niger – mmoja kutoka eneo la Magharibi karibu na Mali na Burkina Faso, na mwingine kutoka Kusini Mashariki katika mpaka wa Nigeria.

Katika taarifa iliyosomwa kwa umma katika runinga, serikali ya Niger ilisema kundi la wapiganaji hao bado halijafahamiki na hata gari lililokuwa limewabeba.

“Idadi ya waliokufa imefikia 58, mmoja amejeruhiwa, magari mawili au zaidi kuteketezwa na vitu vinginge kuharibiwa katika shambulio hilo ,” taarifa imeeleza. Serikali pia imetangaza siku tatu za maombolezo kitaifa, kuanzia leo Jumatano.

Chanzo: globalpublishers.co.tz