Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 5 wafariki dunia, 6 wajeruhiwa kwenye ajali ya barabarani eneo la Lari

0fgjhs7tfih85l1av Watu 5 wafariki dunia, 6 wajeruhiwa kwenye ajali ya barabarani eneo la Lari

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Watu 5 wamefariki dunia kwenye ajali ya barabarani iliyofanyika eneo la Nyambari kule Lari kaunti ya KiambuWengine 6 wako katika hali mahututi na wamelazwa katika hospitali ya Kijabe ambapo wanapokea matibabuKamanda mkuu wa polisi eneo hilo Stephen Kirui amesema idara ya trafiki imeanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyoWatu watano wanahofiwa kufariki dunia na wengine sita kujeruhiwa vibaya kwenye ajali ya barabarani eneo la Nyambari, Lari kaunti ya Kiambu asubuhi ya leo.

Majeruhiwa walikimbizwa katika hospitali ya Kijabe ambapo wanapokea matibabu na wamedaiwa kuwa katika hali mahututi.

Ajali hiyo ilihusisha lori na matatu mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 14 kila moja.

Akithibitisha kisa hicho, kamanda mkuu wa polisi Stephen Kirui alisema idara ya trafiki imeanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Kirui pia amewataka madereva kuwa waangalifu ikizingatiwa hali ya anga katika sehemu zingine za nchi mwezi huu wa Julai ni mbovu sana.

"Nimewasiliana na usimamizi wa hospitali ya Kijabe na imethibitishwa kwamba watu 5 walipoteza maisha yao na sita kujeruhiwa vibaya kwenye ajali hiyo," Kirui alisema.

" Ningependa madereva wote wawe makini na waangalifu, hali ya anga sio nzuri maeneo haya, hatutaki kuripoti maafa zaidi kutokana na ajali," Aliongezea Kirui.

Kati ya walipoteza maisha yao, watatu ni wanaume ilhali wawili ni wanawake.

Kwenye taarifa zingine, mama mmoja mwenye umri wa makamo alipoteza maisha yake kaunti ya Homa Bay baada ya kugongwa na lori akiwa amembeba mtoto mgongoni.

Walioshuhudia ajali hiyo walisema Sharon Otieno alifariki dunia papo hapo kutokana na majeraha ya kichwa huku mtoto wake akikimbizwa katika hospitali ya Ndhiwa akiwa na majeraha madogo

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke