Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 497 wapya waambukizwa Kenya

KENYACOVIDr Watu 497 wapya waambukizwa Kenya

Wed, 15 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya nchini Kenya imetangaza ongezeko la watu 497 wapya wenye virusi vya corona.

Idadi hiyo ni ya juu zaidi ya maambukizi kuwahi kushuhudiwa kwa siku tangu ugonjwa huo ulipogunduliwa nchini humo.

Kufikia sasa Kenya ina jumla ya watu 10,791 walioambukizwa virusi vya corona.

Katika taarifa kwa wanahabari siku ya Jumanne kuhusu mwenendo wa hali ya ugonjwa wa Covid-19 nchini Kenya, Katibu mkuu katika Wizara ya Afya Mercy Mwangangi pia alitangaza kuwa watu watano zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika kipindi cha saa 24, na kufikisha 202 idadi ya vifo vy corona.

Kenya yarekodi idadi kubwa zaidi ya wagonjwa wa corona kwa siku

Wakati huohuo, wafanyakazi wa Hospitali ya kujifungua kina mama ya Pumwani mjini Nairobi wamegoma baada ya wahudumu 41 wa hospitali hiyo kupatikana na virusi vya corona.

Kaimu Mkukuruenzi wa Afya Patrick Amoth, amethibitisha idadi ya waliopata maambukizi katika hospitali hiyo na kuongeza kwamba madaktari waliosalia watapimwa.

Alisema kwamba walioambukizwa 41 ni kati ya 290 waliopimwa huku wahudumu wengine 100 zaidi wakiwa wanasubiri kufanyiwa vipimo.

Wafanyakazi waliosalia kutoa huduma katika hospitali hiyo sasa wameonesha wasiwasi wao baada ya kugundulika kwa maambukizi zaidi ya virusi vya corona huku wengine wakisema kwamba wamelazimishwa kusalia kazini licha ya tukio hilo.

"Tuna tatizo kubwa katika hospitali ya kujifungua ya Pumwani ambapo ninafanyakazi. Serikali ilianza kupima wafanyakazi ugonjwa wa Covid-19 na idadi ya wanaopata maambukizi inazidi kuongezeka," amesema mmoja wa wafanyakazi ambaye hakutaka kutambuliwa kwa hofu ya kuadhibiwa.

Sasa wafanyakazi wanaishi kwa hofu kwa sababu ya kukosa kujua ukubwa wa maambukizi katika hospitali hiyo, na hilo pia linaweka kina mama wajawazito waliolazwa hospitalini humo kuwa katika hatari zaidi

Utafiti wabaini Wakenya milioni 2.6 waliugua Covid 19

Utafiti uliofanywa hivi karibuni ulibaini kuwa Wakenya milioni 2.6 tayari wana virusi vya corona, wanasayansi wameeleza baada ya kupima damu iliyotolewa kwa ajili ya protini inayotumika kwenye mfumo wa kinga.

Protini hiyo (antibody) hutengenezwa na mwili kwa ajili ya kushambulia virusi na bakteria, na uwepo wake kwenye damu unaashiria kuwa mtu huyo aliwahi kuwa na maambukizi- hata iwapo hakuwahi kuonesha dalili. Taasisi ya utafiti wa tiba nchini Kenya

Chanzo cha picha, KEMRI

Watafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa tiba nchini Kenya wameunga mkono mfuko wa kuchangia damu uliofanyika nchi nzima kati ya mwezi Aprili tarehe 30 na tarehe 16 Juni.

''Kupimwa kwa antibodies kumeonesha kuwa Wakenya wengi tayari wamepata maambukizi kuliko ilivyokuwa ikibainika katika shughuli za upimaji nchini humo.,'' Ilieleza taasisi ya Kemri mapema wiki hii ikinukuliwa nan a gazeti la the Star nchini Kenya.

Kemri inakadiria kuwa karibu watu 550,000 jijini Nairobi na karibu 100,000 mjini Mombasa, tayari wameugua virusi hivyo na kupona na pengine kupata kinga.

Imeelezwa kuwa baadhi inawezekana waliathirika mapema mwezi Machi kwa kuwa protini hizo zinazopambana na virusi zinaweza kuwa kwenye damu kwa miezi kadhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live