Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 43 wauawa kwenye mapigano Darfur

'Tutapigana Hadi Mwanajeshi Wa Mwisho'   Kiongozi Wa RSF Wa Sudan Watu 43 wauawa kwenye mapigano Darfur

Sat, 27 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapigano makali yameripotiwa Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake, kati ya Jeshi la Kitaifa la Serikali SAF na wanamgambo wa RSF.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Nairobi, Kenya, msemaji wa ofisi ya Kamishna wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Seif Magango amesema hali inazidi kuwa mbaya kwani katika kipindi cha wiki mbili zilizopita watu wapatao 43 wakiwemo wanawake na watoto wameuawa kutokana na mapigano kati ya pande mbili hizo hasimu.

Inaripotiwa kuwa pande zote zinarusha makombora kwenye maeneo ya raia, wengine wakitumia ndege za kivita kwenye makazi ya watu mjini El- Fasher na viunga vyake.

Hali hiyo imemtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk hasa kutokana na kwamba wapiganaji wa RSF wanalenga vijiji vilivyoko magharibi mwa El-Fasher ambako wanaishi raia wa kabila la Zaghawa.

Mapigano ya silaha yalianza huko Sudan Aprili 15 mwaka jana kati ya jeshi la nchi hiyo (SAF) linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan ambaye ni kiongozi wa Sudan na wanamgambo wa Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) ambao kamanda wao ni Hamdan Dagalo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live