Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 42 wameuawa katika mapigano mapya Sudan

Sudan Kusini Watu 42 Watu 42 wameuawa katika mapigano mapya Sudan

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 42 wameuawa akiwemo mlinda amani mmoja wa Umoja wa Mataifa baada ya kutokea mapitano katika eneo la Abyei karibu na Sudan Kusini. Mapigano hayo yametokea baina ya vijana wenye silaha wa jamii ya Twic ya jimbo jirani la Warrap na Ngok Dinka wa jimbo la Abyei.

Rou Manyiel Rou, Afisa Mtawala Mkuu wa Jimbo la Abyei amethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, mashambulizi katika maeneo ya Nyinkuac, Majbong, na Khadian yaliyofanywa na vijana wenye silaha kutoka jamii ya Twic kwa kkushirikiana na vijana wa jamii ya Nuer watiifu kwa kiongozi wao wa kiroho Gai Machiek yamesababisha pia watu 35 kujeruhiwa.

Afisa huyo amenukuu pia matamshi ya Rais Salva Kii aliyotoa hivi karibuni kuhusu mapigano ya eneo hilo na kusema kuwa, mashambulizi haya ya kikatili yameyoratibiwa kitaasisi. Tunalaani vikali jaribio la vijana wa jamii ya Twic na washirika wao wenye silaha la kukaidi agizo la rais lililotolewa hivi karibuni la kumaliza mzozo kati ya Ngok Dinka na watu wa jamii ya Twic.

Agizo la Rais Kiir lililotolewa Januari 18 lilivitaka vikosi vya usalama kumfukuza kutoka jimbo la Warrap kiongozi wa kiroho wa jamii ya Nuer, Gai Machiek na vijana waaminifu kwake kama sehemu ya jitihada za kutatua mzozo kati ya jamii za Ngok Dinka na Twic.

Agizo hilo pia lilivitaka vikosi vya usalama kuwaita na kuwakamata wanasiasa wa jamii zote zinazozozana ambao wanaonekana kuchochea ghasia kati ya jamii hizo mbili.Manyiel alitoa wito wa kutumwa kwa haraka kwa vikosi vya usalama visivyoegemea upande wowote kwenye mpaka kati ya Kaunti ya Twic na Eneo la Utawala la Abyei.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live