Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 400 wapatikana na COVID-19, wengine 7 wapoteza maisha yao

7773706ab7b8ad56 Watu 400 wapatikana na COVID-19, wengine 7 wapoteza maisha yao

Wed, 7 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wizara ya afya imetangaza kwamba watu wengine 400 wamepatikana na virusi vya COVID-19 kutokana na sampo 5,068 zilizofanyiwa vipimo chini ya saa 24 zilizopita.

Habari Nyngine: Mwanafunzi wa KMTC Homa Bay Aliyetoweka Apatikana Akiwa Ameuawa

Kufikia sasa asilimia ya maambukizi ya virusi hivyo nchini imefikia 7.9%.

Kulingana na taarifa kutoka kwa wizara ya afya iliyotolewa Jumanne, Julai 6, kati ya wagonjwa waliopatikana na virusi hivyo 386 ni Wakenya ilhali 14 ni raia wa nchi za kigeni, 220 ni wanaume huku 180 wakiwa wanawake.

Mgongwa mdogo ana umri wa siku 12 ilhali mkubwa ana miaka 97.

Wagonjwa wengine 354 wamepona kutokana na ugonjwa huo, 259 walikuwa chini ya mpango wa utunzi wa nyumbani ilhali 95 walikuwa wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini.

Kwa jumla wagonjwa waliopona nchini ni 29,165 kulingana na takwimu za wizara ya afya.

Kwenye taarifa za kuhuzunisha, wagonjwa 7 walipoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo na kupelekea idadi ya vifo nchini kufikia 3,697 kwa jumla.

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa idadi ya maambukizi ikiwa na visa 155 ikifuatwa na kaunti ya Kilifi kwa visa 43, Uasin Gishu 34, Siaya 21, Kiambu 19, Busia 18, Mombasa 16, Kisumu 13, Nyamira 11, Nakuru 11, Narok 6, Kwale 5, Marsabit 5 na Murang’a 5.

Nyandarua imerekodi visa 4, Nyeri 4, Kisii 4, Homa Bay 4, Bomet 3, Kajiado 3, Kakamega 3, Kitui 3, Kericho 2, Migori 2, Machakos 1, Trans Nzoia 1, Embu 1, Turkana 1, West Pokot na Garissa kisa kimoja kimoja.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke