Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 40 wateketea wakigombania petroli

Petrolll ).jpeg Watu 40 wateketea wakigombania petroli

Sat, 30 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watu 40 wamefariki dunia kwa kuteketea kwa moto wakati wakichota mafuta ya petroli kwenye lori lililopata ajali.

Tukio hilo limetokea Desemba 28, 2023 katika eneo la Totota, Kaunti ya Bong katikati mwa Liberia ambapo idadi ya vifo na majeruhi inakadiriwa kuongezeka.

Inaelezwa kuwa, baada ya lori hilo kupata ajali, wananchi walikusanyika wakiwa na madumu na ndoo na kuanza kuchota mafuta yaliyokuwa yakimwagika ambapo licha ya dereva wa gari hilo kuwakataza, waliendelea na walichokuwa wanakifanya.

Muda mfupi baadaye, ulitokea mlipuko mkubwa na kusababisha maafa makubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live