Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 36,000 wapoteza makazi bwawa likivunjika Ghana

Ghana Bwawa Kuvunjika.jpeg Watu 36,000 wapoteza makazi bwawa likivunjika Ghana

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 36,000 wamepoteza makazi yao na takriban nyumba 150 zimezama chini ya maji baada ya kutokea mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kupasuka Bwawa la Vilta, kusini mwa Ghana.

Seji Saji Amedonu, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Kukabiliana na Majanga nchini Ghana kwa kifupi (NADMO), amethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, jamii za watu wa vijijini zilizoathiriwa na janga hilo ziko katika wilaya nane za mikoa mikubwa ya Accra, Volta na Mashariki.

Amedonu amesema kuwa janga hilo limetokea baada ya maji mengi kumwagika kutoka kwenye bwawa hilo, ambako kulianza mwanzoni mwa Oktoba, na maji mengi kupita kiasi yaliyotokana na mvua kubwa za mwezi Septemba yalipofanya hali kuwa mbaya zaidi na kulipasua kabisa bwawa hilo.

Miundombinu mingi imeharibiwa yakiwemo pia mashamba, barabara, skuli, vituo vya afya na vituo vya umeme ambavyo vimezama chini ya maji na hadi hivi sasa haijajulikana ni hasara kubwa kiasi gani imesababishwa na janga hilo.

Taarifa zinasema kuwa takriban vijiji 150 vimefunikwa na maji kutokana na mafuriko huko Ghana

Shirika la Taifa la Kukabiliana na Majanga nchini Ghana (NADMO) limewapa hifadhi watu wengi waliokimbia makazi yao katika maeneo ya skuli, Misikitini, makanisani na kwenye mahema. Huduma za maji ya kunywa zinatolewa kupitia matangi maalumu katika wilaya nane tangu mafuriko hayo yalipotokea.

Katika sehemu moja ya taarifa yake, Seji Saji Amedonu amesema: "Tunashirikiana na Idara ya Huduma ya Afya ya Ghana na kurugenzi za afya za wilaya katika wilaya hizi zote ili kutoa huduma za afya kwa watu walioathirika. Tuna zaahanati zetu zinazotembea katika takriban wilaya zote zilizoathirika."

Ameongeza kuwa, hali ya kawaida inatarajiwa kurejea ndani ya wiki mbili hadi tatu zijazo. Baada ya hapo ndipo zoezi la usafi, kupiga dawa na kufanya uchunguzi wa afya litaanza ili kurahisisha kurejea watu katika makazi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live