Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 32 wameuawa katika mapigano makali ya kikabila Sudan Kusini

Sudan Jeshiiii Malalamikp Watu 32 wameuawa katika mapigano makali ya kikabila Sudan Kusini

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 32 wameuawa katika mapigano makali yaliyozuka jana kwenye mpaka wa Sudan Kusini na eneo linalozozaniwa la Abyei.

Arou Manyiel Arou, katibu mkuu katika ofisi ya msimamizi wa eneo la kiutawala la Abyei amethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, ghasia hizo zilizuka mapema jana asubuhi kufuatia shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya watu wa kabila la Dinka huko Wuncuei na maeneo ya Nyiel ya eneo la kiutawala la Abyei. Shambulizi hilo la kulipiza kisasi limefanywa na vijana wenye silaha kutoka Kaunti ya Twic inayopakana na jimbo la Warrap la Sudan Kusini.

Amesema washambuliaji hao waliotoka eneo la Ajak-Kuach waliripotiwa kusaidiwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanajeshi wa Kikosi cha Ulinzi cha Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF).

Alipohojiwa na shirika la habari la Xinhua, Arou amesema: "Baadhi ya watu wa eneo hilo wamewaona washambuliaji hao wakiwa wamevaa sare za Jeshi la Wananchi wa Sudan Kusini. Watu wengi wakiwemo watoto na wanawake wameuawa na 27 wamejeruhiwa."

Shambulizi la hivi sasa la kulipiza kisasi limetokea baada ya mapigano ya wiki iliyopita katika eneo la Ayuok kati ya pande hizo mbili, ambayo yalisababisha watu 34 kuuawa akiwemo mwanajeshi mmoja wa Sudan Kusini. Jamii hizo zimekuwa zikigombea kwa miaka mingi umiliki wa kipande cha ardhi katika eneo la mpaka la Aneet, ambalo linatenganisha jamii hizo mbili.

Abyei imeendelea kuwa eneo lenye mzozo mkubwa kati ya Sudan Kusini na jirani yake Sudan ambayo kwa sasa imekumbwa na mgogoro mkubwa wa ndani tangu Aprili 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live