Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 31 wafariki wakati wa zoezi la kugawa vyakula kanisani

Chakula Kanisani Watu 31 wafariki wakati wa zoezi la kugawa vyakula kanisani

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 31 wameripotiwa kufariki na wengine 7 kujeruhiwa wakati wa mkanyagano wa kugawa chakula kanisani Nchini Nigeria, ambapo shuhuda mmoja wa tukio alishuhudia mama mjamzito na watoto kadhaa wakiwa sehemu ya waliofariki, jana Mei 28, 2022.

Msemaji wa Polisi, Grace Iringe-Koko anasema tukio la kugawa chakula liliandaliwa na Kanisa la Kings Assembly Pentecostal katika Jimbo la Rivers ambalo hufanyika kila mwaka likiewa jina la “Duka la Bure” ikiwa ni sehemu ya mpango wao kusaidia jamii.

Tukio lilitakiwa kuanza saa 3:00 Asubuhi lakini idadi kubwa ya watu ilifika mapema kuanzia saa 11:00 Alfajiri ili kupanga mstari, wingi wa watu ukasababisha mvurugano na mwisho mkanyagano ukaanza.

Polisi wanaendelea na uchunguzi kujua nini hasa kilikuwa chanzo kwa kuwa zoezi hilo lililazimika kuahirishwa kutokana na vurugu kutokea. Inaelezwa kuwa kuna watoto watano wa familia moja walikuwa miongoni mwa waliopoteza maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live