Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 300 wafariki, nyumba 300 zasombwa na mafuriko Bujumbura

Burundi Dgv Watu 300 wafariki, nyumba 300 zasombwa na mafuriko Bujumbura

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka nchini Burundi imewaamuru watu wanaoshi mwambao mwa Ziwa Tanganyika Bujumbura kuhama ndani ya wiki mbili kutokana na mafuriko yanayosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya mvua kunyesha kwa siku mbili mfululizo na kusababisha maafa makubwa ikiwemo watu watatu kupoteza maisha yao, nyumba zaidi ya mia tatu zikibomoka huku watu watano wakiwa hawajulikani walipo.

Wanaotakiwa kuhama ni wananchi wanaoishi maeneo ya Gatumba Bujumbura vijijini ambao takribani nyumba zaidi ya 200 zimebomoka kutokana na mvua zilizonyesha wiki hii.

Uongozi umefahamisha kuwa nyumba hizo mia tatu zilizosombwa na maji ni kutoka katika Kata ya Gatumba na Kibenga huku uokoaji ukindelea kufanyika.

Meya wa jiji la Bujumbura Jimmy Hatungimana na Mkuu wa Mkoa wa Bujumbura vijijini, Desire Nsengiyumva wamesema kuwa watu wanapaswa kuhama ndani ya wiki mbili serikali ikiwa inaangalia namna ya kuwasaidia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live