Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 30 hawajulikani walipo Nigeria

Nigeria 30 30 Watu 30 hawajulikani walipo Nigeria

Wed, 25 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watu 30 hawajulikani walipo Kaskazini Mashariki mwa jimbo la Borno nchini Nigeria, baada ya kushambuliwa na vikosi vya watu wenye silaha week end iliyopita.

Mashuhuda wanasema kuwa waathirwa wa tukio hilo wanatokea mji wa  Rann , ambapo walifyatuliwa risasi na watu wenye silaha ambao walikua kwenye pikipiki., wakati walipokua porini kutafuta kuni.

Kuna hofu kwamba makumi ya watu wametetwa ama wameuawa 

Haijulikani ni nani aliyefanya shambulizi hilo, lakini vikosi vya Boko Haram na vingine vinavyohusiana na dola la kiislamu IS vimekua vikisababisha matukio ya aina hiyo kwenye ukanda huo.  

Mamlaka za kijeshi za Nigeria hazijatoa tamko lolote kuhusiana na tukio hilo.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live