Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 3 wauawa katika maandamano Senegal

Senegal: Vurugu Zaenea Baada Kuahirishwa Kwa Uchaguzi Mpaka Mwezi Desemba Watu 3 wauawa katika maandamano Senegal

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wasiopungua watatu wameuawa katika mapigano ya wiki iliyopita kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama kuhusu kuahirishwa uchaguzi wa rais nchini Senegal, vyombo vya habari vya ndani viliripoti jana Jumapili.

Maandamano makali yalizuka kote nchini Senegal Ijumaa iliyopita, yakiongozwa na vyama vya siasa vya upinzani na baadhi ya mashirika ya kiraia yanayopinga kucheleweshwa kwa uchaguzi.

Waliouawa ni pamoja na mwanafunzi wa shule ya upili aliyekuwa na umri wa miaka 19, muuza duka Modou Gueye aliyekuwa na umri wa miaka 23 na mwanafunzi wa chuo kikuu.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Senegal, Sidiki Kaba, amekanusha ripoti za vyombo vya habari kuwa askari usalama walihusika na vifo hivyo.

Mnamo Februari 3, Rais wa Senegal, Macky Sall, alitangaza kuahirishwa uchaguzi wa rais, akitaja sababu kuwa ni mzozo kuhusu orodha ya wagombea na madai ya ufisadi wa majaji wa kikatiba. Rais wa Senegal Macky Sall

Bunge la Kitaifa la Senegal wiki iliyopita liliunga mkono muswada wa kuahirisha uchaguzi wa rais wa Februari 25 hadi Desemba 15, wakati wa kikao cha mvutano ambapo wabunge wa upinzani waliondolewa kwa nguvu kutoka katika chumba hicho.

Baraza la Katiba linatarajiwa kutoa uamuzi katika takriban baada ya wiki moja kuhusu suala hilo.

Karim Wade, mwana wa kiume wa rais wa zamani wa Senegal, na mpinzani mashuhuri wa serikali ya sasa ya Senegal, Ousmane Sonko ni miongoni mwa shakhsia walioondolewa kwenye orodha hiyo ya wagombea wa kiti cha urais.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imewataka wanasiasa wa Senegal kujiepusha na ghasia na vitendo vingine vinavyoweza kudhoofisha amani na utulivu, baada ya tangazo la kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais kuibua maandamano nchini humo.

Katika taarifa, ECOWAS imesema inafuatilia hali hiyo kwa wasiwasi na hivyo imewakumbusha wanasiasa jukumu lao katika kudumisha amani na utulivu katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live