Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 28 wauawa, 46 wajeruhiwa katika mapigano Sudan

Ulimwengu Unapuuza Hatari Ya Mauaji Ya Kimbari Sudan   Mtaalam Wa UN Watu 28 wauawa, 46 wajeruhiwa katika mapigano Sudan

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban raia 28 wameuawa na wengine 46 wamejeruhiwa katika shambulio lililofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko El Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini magharibi mwa Sudan.

Katika taarifa yake ya jana Jumapili, Al-Hafiz Bakheet, kaimu gavana wa jimbo la Darfur Kaskazini amesema: "Wanamgambo wa RSF wamefanya mauaji mapya baada ya kushambulia mara kwa mara masoko na maeneo ya raia, na kuvamia nyumba za wananchi na kuiba kila kitu.

Kwa mujibu wa gavana huyo, vikosi vya Jeshi la Sudan (SAF) kwa kushirikiana na kikosi cha wanaharakati wenye silaha wa eneo la Darfur wamefanikiwa kuzima mashambulizi ya RSF na kuwasababishia hasara kubwa. Hakuna ishara zozote za kumalizika vita hivi karibuni huko Sudan

Pia amesema: "El Fasher itaendelea kupambana kiume na kutotetereka na karibuni hivi itawasafisha waasi wote."

Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) havijatoa matamshi yoyote kuhusiana na taarifa juu ya shambulio hilo.

Tangu tarehe 10 Mei mwaka huu, mapigano makali ya uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi yamekuwa yakiendelea kati ya wale majenerali wanaoongoza kundi la SAF na wale wanaoongoza kundi la RSF na wahanga wakuu wa vita hivyo vya uchu wa madaraka ni raia wa kawaida.

Sudan imekuwa ikishuhudia mzozo mbaya kati ya SAF na RSF tangu Aprili 15, 2023. Umoja wa Mataifa unasema: Watu wasiopungua 16,650 wamesharipotiwa kuuawa katika vita hivyo. Takriban watu milioni 10.7 ni wakimbizi wa ndani, huku takriban wengine milioni 2.2 wamekimbilia nje ya Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live