Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 264,402 wameshapata dozi kamili ya Corona Uganda

D62e458abffceab4f9f4ed287e384305 Watu 264,402 wameshapata dozi kamili ya Corona Uganda

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WANANCHI 264,402 wa Uganda wamepata dozi kamili kwa kuchanjwa mara mbili chanjo dhidi ya ugonjwa wa virusi vya corona (Covid-19) hadi kufikia wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Afya nchini hapa, waliochanjwa mara mbili na kukamilisha dozi dhidi ya Covid-19 ni wahudumu wa afya 43,957 kati ya 150,000, maofisa usalama 47,148 kati ya 250,000 na walimu 61,848 kati ya 550,000.

Aidha, takwimu hizo za wizara zinaonesha kuwa, wananchi 56,912 wenye umri wa miaka 50 na zaidi, na wengine 6,373 wanaoishi na magonjwa mbalimbali wamepewa chanjo kamili.

Serikali ilikuwa imepanga kuchanja zaidi ya watu milioni nne katika makundi mbalimbali ya vipaumbele dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Meneja wa Usimamizi wa Programu ya Kinga wa Uganda (UNEPI), Dk Alfred Driwale, alisema kama nchi hiyo ingekuwa na chanjo zaidi, watu wengi wangekuwa wamepewa chanjo kamili hadi sasa.

"Suala pekee tunaloshughulikia sasa ni kuwa na chanjo za kutosha. Hilo ndilo suala kubwa kwa sasa. Pamoja na uhaba wa chanjo duniani, nchi kama Uganda hazijaweza kununua chanjo na tunategemea misaada," alisema Dk Driwale.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, hadi sasa serikali imepokea ufadhili wa dozi 2,024,600 za chanjo zikiwemo 1,724,600 za chanjo aina ya AstraZeneca zilizotolewa kupitia Kituo cha COVAX na dozi 300,000 za Sinovac kutoka China.

Driwale alisema wanatarajia kutoa chanjo zaidi baada ya kuingia nchini kwa chanjo zitakazonunuliwa mwezi huu. Tayari wameshanunua dozi milioni 27 za chanjo za Johnson & Johnson zinazotolewa mara moja na Sinopharm.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live