Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 22 wafariki katika ajali ya barabarani kaskazini mwa Senegal

Watu 22 Wafariki Katika Ajali Ya Barabarani Kaskazini Mwa Senegal Watu 22 wafariki katika ajali ya barabarani kaskazini mwa Senegal

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: Voa

Watu 22 walifariki Jumatatu wakati basi na lori yalipogongana kaskazini mwa Senegal, wafanyakazi wa zima moto wamesema, wiki moja baada ya ajali kati ya mabasi mawili yalisababisha vifo vya watu 40.

Zaidi ya watu 20 walijeruhiwa katika ajali hiyo ambayo ilitokea karibu na Sakal eneo la Louga, Papa Ange Michel Diatta, kanali anayefanya kazi na idara ya kitaifa ya zima moto ameiambia AFP.

Waziri mkuu Amadou Ba alilitembelea eneo la ajali akiapa kuimarisha sheria mpya za barabarani.

Basi hilo lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 32 lakini lilikuwa limebeba watu 47, Ba aliwaambia waandishi wa habari, akisema kutoheshimu sheria za barabarani kunaongeza idadi ya vifo.

Rais Macky Sall aliandika kwenye Twitter” Ajali nyingine mbaya kwenye barabara zetu.”

Ameongeza kuwa idadi hiyo ya vifo inaonyesha umuhimu wa kuimarisha sheria za usalama wa barabarani.

Ajali za barabarani ni jambo la kawaida nchini Senegal, hasa kutokana na uzembe wa madereva, barabara mbovu na uchakavu wa magari, wataalam wanasema.

Senegal iliingia kwenye siku tatu za maombolezo baada ya mabasi mawili kugongana mapema asubuhi tarehe 8 Januari katika eneo la katikati la Kaffrine, na kusababisha vifo vya watu 40 na zaidi ya 100 kujeruhiwa.

Chanzo: Voa