Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 20 wauawa katika shambulio Mali

Mali Watu 20 wauawa katika shambulio Mali

Mon, 20 Jun 2022 Chanzo: BBC

Karibu watu 20 wameuawa katika shambulio linaotuhumiwa kutekelezwa na wapiganaji wa kijihadi kaskazini mwa Mali, ofisi ya kikanda katika eneo hilo inasema.Ghasia za Jumamosi zilitokea karibu na mji wa Gao.

Afisa huyo aliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba hali ilikuwa tete kwani raia walikuwa wakitoroka wakati wanamgambo hao walipokuwa wakifanya unyama dhidi yao.

Umoja wa Mataifa unasema hali ya usalama katika maeneo ya Gao na Ménaka imezorota vibaya.

Mapema Jumapili walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliuawa karibu na mgodi mmoja huko Kidal kaskazini mwa nchi.

Chanzo: BBC