Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 20 wateketea wakichota mafuta

Motooootrs Watu 20 wateketea wakichota mafuta

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban zaidi ya watu 20 wanaripotiwa kufariki dunia kwa kuungua moto baada ya mlipuko wa lori la mafuta kutokea Jumapili asubuhi Oktoba 1, barabara ya Benin -Sapele kati ya Ologbo Jimbo la Edo na Koko Jimbo la Delta.

Watu hao walijaribu kuchota mafuta kwenye lori lililosheheni lita 30,000 za mafuta baada ya kuacha njia yake na kuanguka na kumwaga mafuta eneo hilo ikiwa ni maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Nigeria.

Baadhi ya watu walikimbilia kuchota mafuta licha ya kuonywa na madereva na watu wa usalama na kuvamia eneo la tukio baada ya kupata taarifa za ajali hiyo, Afisa Uhusiano wa Umma wa Polisi wa jimbo hilo, DSP Bright Edafe alithibitisha tukio hilo katika taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari .

Edafe alisema zaidi ya magari 20 pikipiki moja yameteketea kabisa huku moto ukiwaka bila kudhibitiwa wakati wa mlipuko huo.Shahidi aliyejionea tukio hilo ambaye alizungumza na Daily Trust alisema: "Tulijaribu kuwazuia lakini hawakusikia na kutupatia vitisho, Walikuja kwa wingi wakiwa wamebeba kila aina ya vyombo kutaka kuchota mafuta yaliyomwagika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live