Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 20 wafariki Kenya baada ya mafuriko kusomba makazi huko Mai Mahiu

Kenya: Watu Zaidi Ya 50 Wamefairki Kutokana Na Mafuriko Watu 20 wafariki Kenya baada ya mafuriko kusomba makazi huko Mai Mahiu

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Watu 20 wamethibitishwa kufariki baada ya mafuriko makubwa kusomba nyumba kadhaa katika Kijiji cha Kamuchiri Mai Mahiu, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya kufuatia mvua kubwa iliyonyesha.

Maji ya mafuriko yalitoka kwenye mto ulio karibu ambao ulivunja kingo zake Jumapili usiku, kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya.

Kamanda wa polisi wa Naivasha Stephen Kirui amethibitisha kisa hicho akibainisha kuwa wengine kadhaa wamekimbizwa katika hospitali ya Naivasha kwa matibabu.

Chanzo: Bbc