Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 20 Wafariki kwa Corona Kenya, Vifo Vyafikia 2,244

Kenya Corona?fit=680%2C382&ssl=1 Watu 20 Wafariki kwa Corona Kenya, Vifo Vyafikia 2,244

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Watu 20 Wafariki kwa Corona Kenya, Vifo Vyafikia 2,244 April 6, 2021 by Global Publishers



Watu 20 zaidi wamefariki ndani ya saa 24 kutokana na kupata Virusi vya Corona na kufanya idadi ya watu waliofariki kwa Corona nchini #Kenya kufikia 2,244.

Aidha watu 460 wameripotiwa kuthibitika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo katika saa 24 zilizopita idadi inayofanya walioambukizwa kufikia 139,448.

Wizara ya Afya imetangaza watu 178 kuwa wamepona 79 kati yao wakiwa ni wale waliokuwa wakijitibia nyumbani na hivyo idadi ya watu waliopona imefikia 94,361.

Watu 1,590 wapo chini ya uangilizi wa kitabibu katika vituo vya afya na wengine 5,998 wanatibiwa majumbani mwao wakiwa wamejitenga, 200 wanapatiwa matibabu wakiwa katika hali mbaya na wamewekewa Oksijeni.

Chanzo: globalpublishers.co.tz