Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 18 wauawa kwa risasi Afrika Kusini

South Africa Police Shout Watu 18 wauawa kwa risasi Afrika Kusini

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi katika jimbo la Limpopo la kaskazini mashariki mwa Afrika Kusini wametangaza kuwa wamewapiga risasi na kuwaua watu 18 waliokuwa na silaha.

Maafisa wa polisi wa Afrika Kusini wamesema kuwa walilazimika kuwafanyatulia risasi watu ambalo walikuwa na nia ya kuteka gari moja lililokuwa limebeba fedha.

Katika taarifa yake, jeshi hilo la Polisi la Afrika Kusini limesema kuwa, mara baada ya kuwasili polisi katika eneo hilo, kundi hilo la majambazi lilianza kuwafyatulia risasi polisi ambao nao walilazimika kujibu mashambulizi hayo.

Ufyatulianaji risasi baina ya maafisa wa polisi na majambazi hao uliendelea kwa muda wa nusu saa na kupelekea kuuawa wanaume 16 na wanawake wawili. Vitendo vya ujambazi vimeongezeka sana nchini Afrika Kusini

Fannie Masemola, Kamishna wa Polisi wa jimbo la Limpopo ambalo liko umbali wa takriban kilomita 430 kaskazini mashariki mwa Johannesburg amewaambia waandishi wa habari kuwa, afisa mmoja wa polisi amejeruhiwa kwenye ufyatulianaji risasi huo.

Mwaka jana pia majambazi 10 waliuawa wakati walipojaribu kusimamisha gari la kusafirishia fedha. Majambazi hao waliuawa baada ya kuifyatulia risasi halikopta ya polisi na kumjeruhi rubani wake.

Mwezi Mei mwaka huu, Bhekokwakhe "Bheki" Hamilton Cele, Waziri wa Polisi wa Afrika Kusini alisema kuwa, mashambulio dhidi ya magari yanayosafirisha fedha yameongezeka kwa asilimia 20 nchini humo na mashambulizi 64 kati ya hayo yametokea kwenye miezi mitatu ya mwanzoni mwa mwaka huu wa 2023.

Takwimu za vitendo vya uhalifu ambazo huwa zinatangazwa mubashara na jeshi la polisi kwenye televisheni za Afrika Kusini zinaonesha kuwa, katika miezi ya hivi karibuni nchi hiyo imekuwa na kiwango kikubwa cha uhalifu duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live