Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 17 washukiwa kufariki kwa gesi Afrika Kusini

 Watu 17 Washukiwa Kufariki Kwa Gesi Afrika Kusini Watu 17 washukiwa kufariki kwa gesi Afrika Kusini

Thu, 6 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Uvujaji wa hewa ya gesi ya nitrate oxide nchini Afrika Kusini unashukiwa kusababisha vifo vya watu 17, maafisa wa eneo hilo wanasema.

Wengine kumi na watano wanapata matibabu hospitalini huku watatu kati yao wakiwa mahututi. Maafisa wanasema tukio hilo linahusiana na shughuli haramu katikamigodi ya dhahabu

Waathiriwa - ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto - walikufa baada ya kuvuta gesi kwenye makazi yasiyo rasmi katika eneo la Boksburg, mashariki mwa Johannesburg.

Uvujaji huo uliotokea Jumatano umehusishwa na uchimbaji haramu wa dhahabu katika eneo hilo.

Gesi ya nitrate oksidi mara nyingi hutumiwa na wachimbaji haramu wa dhahabu - wanaojulikana nchini kama zama zamas - kuchimba dhahabu kutoka kwenye udongo ulioibwa kutoka katika mashimo ya migodi yaliyotelekezwa.

Moja ya mitungi ya gesi ilipatikana ikivuja katika mji wa Angelo wenye wakazi wengi wa Boksburg.

Waathiriwa walipatikana ndani ya eneo la mita 100 (futi 328) kutoka eneo la tukio.

Hakuna mtu aliyeweza kupelekwa hospitalini, maafisa wa huduma ya dharura wameambia BBC.

Lakini wanahofia miili zaidi inaweza kupatikana huku timu za uokoaji zikiendelea na kazi yao.

Mkasa huu unakuja miezi sita tu baada ya lori la gesi kulipuka katika mkesha wa Krismasi na kusababisha vifo vya watu 41 katika mji huo huo.

Chanzo: Bbc