Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 17 wafariki katika maandamano Congo

Maandamano Kongo Watu 17 wafariki katika maandamano Congo

Wed, 27 Jul 2022 Chanzo: BBC

Raia 12, polisi wawili na mwanajeshi mmoja wa kikosi cha walinda amani cha MONUSCO wameuawa katika ghasia za maandamano na uporoji dhidi ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa katika DRC.

Kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, MONUSCO, wakimesema kuwa mwanajeshi mmoja na polisi wawili wa waliuawa waliposhambuliwa na wanamgambo wenye silaha. Mwanajeshi mmoja wa MONUSCO pia amejeruhiwa vibaya.

Katika taarifa yake, MONUSCO inasema kuwa shambulio la Jumanne lililofanywa dhidi ya makazi ya kituo cha wanajeshi wake kilichopo katika mji wa Butembo katika jimbo la Kivu Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

MONUSCO inasema washambuliaji waliwanyang’anya polisi wa wake bunduki, wakawapiga risasi kwa karibu walinda amani wa MONUSCO.

Jumanne waandamanaji walikuwa na hasira kufuatia kuuawa kwa wenzao tangu yalipoanza maandamano ya ghasia Jumatatu.

Kiongozi wa mpito wa MONUSCO, Khassim Diagne, yalipinga taarifa za vyombo vya habari kwamba wanajeshi wa MONUSCO waliwapiga risasi raia.

Chanzo: BBC