Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 15 wauawa na wanamgambo Ituri DRC

Shambulizi La Kuvizia Lafanyika DRC Watu 15 wauawa na wanamgambo Ituri DRC

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 15 wameuawa katika shambulio linalohusishwa na wanamgambo wa kundi la CODECO huko Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, vyanzo vya ndani na jeshi vimesema siku ya Jumatatu.

Wanamgambo wa CODECO wamefanya shambulio kwenye kambi ya wavuvi huko Gobu, siku ya Jumapili, Charité Banza, kiongozi wa mashirika ya kiraia huko Bahema Nord, katika jimbo la Bahema, amesema kulingana na shirika la habari la AFP.

Shambulio hilo lilidumu "zaidi ya saa mbili tu na kuua takriban watu kumi na watano", amesema, huku akitoa wito kwa vikosi vya jeshi la DRC kukabiliana vilivyo na makundi yenye silaha.

"Wanamgambo hawa hawashambuliwi wala kukamatwa," Banza amesema.

Ni "raia tisa, askari na wanamgambo wanne wa CODECO wameuawa", ameeleza Pilo Mulindo, mkuu wa eneo la Bahema Kaskazini, na kubaini kwamba idadi hii ni ya muda kwa sasa.

Akihojiwa na shirika la habri la AFP, Luteni Jules Ngongo, msemaji wa jeshi, pia amelishutumu kundi laCODECO kwa "kuwavamia raia waliokuwa katikati ya maombi Jumapili katika kanisa lao la Gobu, mwambao wa Ziwa Albert", mpakani na Uganda.

"Wanajeshi wetu walijibu shambulio hili, wanamgambo hawa wanafuatiliwa ," ameongeza, bila kutoa idadi rasmi ya vifo.

CODECO ni kundi la wanamgambo wengi ambao wanadai kulinda kabila la Lendu dhidi ya kabila hasimu, Hema, pamoja na jeshi la DRC.

Mashambulizi ya CODECO na wanamgambo wengine wa kikabila hutokea mara kwa mara huko Ituri, hasa kaskazini mwa Bunia, mji mkuu wa mkoa huo.

Wiki moja kabla, watu wengine saba waliuawa katika eneo hilo, Bwana Banza amekumbuka.

Baada ya muongo mmoja wa utulivu, mzozo mbaya huko Ituri kati ya makabila ya Hema na Lendu umeanza tena tangu mwisho wa mwaka 2017, na kusababisha vifo vya maelfu ya raia na watu zaidi ya milioni moja na nusu kuyatoroka makaazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Mgogoro wa awali kati ya wanamgambo wa kikabila ulisababisha maelfu ya vifo kati ya mwaka 1999 na 2003, hadi kuingilia kati kwa kikosi cha Ulaya, Operesheni Artemis, chini ya usimamizi wa Ufaransa.

Makundi mengi yenye silaha, ambayo wakati mwingine yanaungwa mkono na nchi jirani, yamekuwa yakiendelea kwa miongo mitatu mashariki mwa DRC, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live