Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 15 wauawa katika mlipuko wa bomu mashariki mwa DRC

UN MAANDAMANO DRC Watu 15 wauawa katika mlipuko wa bomu mashariki mwa DRC

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa akali watu 15 wamefariki dunia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya watoto kupeleka nyumbani kwao kifaa cha kuripuka walichokiokota michezoni mwao.

Mkasa huo ulitokea katika kijiji cha Kyangitsi kilichopo eneo la Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini. Afisa mmoja kutoka katika asasi za kiraia katika eneo hilo, Telesphore Mitondeke, amesema wakaazi wa huko ndio walioweza kubaini kuwa bomu limeripuka baada ya mkasa huo.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, majuma mawili yaliyopita, eneo hilo limekuwa la mapigano kati ya vikundi vya wenyeji wenye silaha vinavyogombea udhibiti wa vijiji, ambapo tayari maeneo mengi yameingia mikononi mwa kundi lijiitalo Wazalendo.

Wakati huo huo, Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo amerejesha fomu ya kugombea tena nafasi hiyo kwa muhula wa pili, akijiunga na orodha ndefu inayojumuisha wanasiasa mashuhuri. Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo

Tshisekedi, aliyeingia madarakani baada ya uchaguzi wa mwaka 2018, aliwasilisha rasmi fomu za kuwania urais kwa miaka mingine mitano mjini Kinshasa siku ya Jumamosi (Oktoba 7).

Kwa hatua hiyo, anaungana na wagombea wengine zaidi ya kumi, wakiwemo wanasiasa wakubwa na mawaziri wa zamani serikalini, ingawa wengi wanaamini upinzani umekuwa dhaifu sana kutokana na kugawanyika kwake.

Utawala wa Rais Tshisekedi umekumbwa na hali ngumu ya uchumi, janga la Covid 19, mlipuko wa Ebola, ukosefu wa usalama hasa mashariki ya nchi ambako wapiganaji wa kundi la M23 waliteka sehemu ya maeneo ya mashariki na kusababisha kuvunjika kwa uhusiano na Rwanda.

Tshisekedi, kijana wa mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Etienne Tshisekedi, aliyeahidi kupambana na ulaji rushwa na utawala wa kimabavu anakanusha tuhuma kutoka makundi ya kutetea haki za binadama na wakosowaji wake, kwamba ameshindwa kutekeleza ahadi zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live