Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 15 wauawa katika 'mashambulizi Burkina Faso

Burkina Faso Magaidiii 53 Watu 15 wauawa katika 'mashambulizi Burkina Faso

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia 15, wakiwemo wasaidizi watatu wa jeshi, waliuawa katika "mashambulizi yaliyotokea kwa wakati mmoja" na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi siku ya Jumamosi mashariki mwa Burkina Faso, shirika la habari la AFP limeripoti siku ya Jumanne kutoka kwa vyanzo vya ndani na usalama.

"Mashambulizi haya yaliyofanyika kwa wakati mmoja" yalitokea katika vitongoji viwili vya Diapaga, mji mkuu wa jimbo la Tapoa, katika eneo la Mashariki, na kusababisha vifo vya watu kumi na watano, mkazi wa eneo hilo ameliiambia shirika la habari la AFP, shambulio na idadi ya vifo iliyothibitishwa na mwakilishi wa mashirika ya kiraia katika mkoa huo.

"Watu kumi na tano, ikiwa ni pamoja na wasaidizi watatu wa jeshi (VDP) na raia kumi na wawili walipigwa risasi na watu wasio na imani au sheria", ambao "waliongoza mashambulizi haya", inabaini barua iliyoandikwa na msemaji wa mashirika ya kiraia, Kondia Pierre Yonli.

Kwa kuuthibitisha shambulio hilo, chanzo cha usalama kimebaini kwamba "mwitikio wa vikosi vya ulinzi ulifanya iwezekane kuwafukuza washambuliaji na kuwaangamiza makumi kadhaa." "Operesheni ya ardhini inaendelea katika eneo la mashariki na tayari imewaangamiza magaidi zaidi ya hamsini na kubomoa kambi zao kadhaa," chanzo hiki kimesema.

Tangu mwaka 2015, Burkina imekumbwa na ghasia zinazofanywa na makundi ya wanajihadi yenye mafungamano na Islamic State na Al-Qaeda ambayo tayari yalikuwa yakishambulia nchi jirani za Mali na Niger. Hadi sasa, mashambulizii hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 17,000, wakiwemo wanajeshi katika kipindi cha miaka minane, ikiwa ni pamoja na zaidi ya watu 6,000 tangu kuanza kwa mwaka 2023, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la ACLED ambalo linaorodhesha waathirika wa migogoro duniani kote.

Vurugu hizi pia zimesababisha zaidi ya watu milioni mbili kuyahama makazi yao ndani ya nchi, kulingana na Baraza la Kitaifa la Misaada ya Dharura na Urekebishaji (CONASUR).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live