Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 14 wauawa wakiwa baa

Watu 14 Wauawa.jpeg Watu 14 wauawa wakiwa baa

Sun, 10 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 14 wamefariki dunia na wengine tisa wamejeruhiwa baada ya watu wenye silaha kufyatua risasi kwenye baa mjini Soweto nchini Afrika Kusini.

Polisi nchini humo wamesema shambulizi hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo Jumapili Julai 10, 2022 ambapo baada ya washambuliaji hao kufanya mauaji walitoweka kwa kutumia gari.

Wamesema watu tisa waliojeruhiwa hali zao ni mbaya ambapo wako haspitalini wakiendelea kupatiwa matibabu.

Mkuu wa Polisi wa eneo la Gauteng, Luteni Jenerali Mawela amesema kuwa ufyatuaji risasi huo unaonekana kuwa "shambulio la damu kali dhidi ya walinzi wasio na hatia wa baa" na kwamba sababu ya ufyatuaji huo bado haijajulikana.

Kwa mubiju wa vyombo vya ndani vya Afrika Kusini, tukio hilo limetokea wiki mbili tu baada ya vijana wengine 21 kukutwa wamekufa kwenye baa katika eneo lingine la East London nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live