Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 130 wafariki kwa mafuriko Sudan

WhatsApp Image 2022 09 17 At 1.jpeg Mafuriko Sudan

Sun, 18 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watu 130 wamefariki dunia na wengine kadhaa wamenusurika kifo kwa sababu ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko nchini Sudan.

Mafuriko hayo yamesababisha uharibu mkubwa katika makazi ya watu ambapo inakadiria kuwa zaidi ya nyumba 128,000 zimeharika na kwamba tayari serikali imetangaza hali ya dharura katika majimbo 18 ya nchi hiyo.

Ripoti inaeleza kumekuwa na ongezeko la vifo vya watu kutoka 112 hadi 134 ndani ya mwezi huu huku Jimbo la Kordofan lililopo Kaskazini mwa nchi hiyo likiongoza kwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, majimbo mengine yaliyoathiriwa na mafuriko hayo ni Gedaref, Kassala na Darfur.

Shirika hilo linahofia kuwa hadi kufikia mwisho wa mwaka huu huenda watu 460,000 wakaathiriwa na mafuriko hayo nchini Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live