Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 12 wauawa katikamashambulizi Congo

Congo Dr 12 Tena Watu 12 wauawa katikamashambulizi Congo

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watu 12 wameuawa huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika mashambulizi yaliyotokea mashariki mwa nchi hiyo siku 3 zilizopita.

Kiongozi mmojawapo wa jeshi katika jimbo la Kivu kaskazini ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa kuna mwanajeshi mmoja aliuawa katika shambulio kaskazini mwa mji wa Butembo na wanamgambo wa mai-mai , pia aliongezea kuwa wapiganaji wengine wawili wa kundi hilo waliuawa katika shambulio hilo.

Jana Rais wa mashirika ya kiraia huko Lodjo katika jimbo la Huri prince Kaleta wakati akizungumza na shirika la habari la ASP, alisema kuwa wachimba madini wengine sita waliuawa kwa kukatwa vichwa na waasi wa kundi la CODECO.

Raia wengine watatu waliauwa katika shambulio lililofanywa na ADF na waasi usiku wa jumamosi katika jimbo la Kivu kaskazini mwa nchi hiyo, Congo inakabiliwa na makundi ya waasi ambao wamekuwa na kasumba ya kuwashambulia raia mara kwa mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live