Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 11 wauawa katika mapigano ya kikabila DRC

Vikosi Munucos DRC Watu 11 wauawa katika mapigano ya kikabila DRC

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wasiopungua 11 wameuwa baada ya kuibuka mapigano makali ya kikabila katika mkoa wa Mai-Ndombe, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Shirika la habari la Reuters limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, watu wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye makabiliano hayo baina ya makabila ya Teke na Yaka.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu zaidi ya 3,000 wameuawa huku wengine zaidi ya 300,000 wakilazimika kuwa wakimbizi kutokana na migogoro ya kikabila katika eneo hilo tokea mwaka 2022.

Chifu wa kijiji, Stany Libie na kiongozi wa kundi la kiraia, Martin Suta wamenukuliwa na Reuters wakithibitisha habari ya kutokea mapigano hayo baina ya wanamgambo wa Mobondo wanaotoka kabila la Yaka na wanakajiji wa kabila la Teke.

Katika hatua nyingine, watu zaidi 40 wameripotiwa kufa maji baada ya boti iliyokuwa imewabeba kuzama katika mkoa wa Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ajali za boti huripotiwa mara kwa mara nchini DR Kongo

Mustafa Mamboleo, afisa wa mkoa wa Kivu Kusini amelinukuliwa na shirika la habari la Anadolu akisema kuwa, matumaini ya familia za wahanga kupata miili ya wapendwa wao waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo yalififia kabisa jana Jumatano.

Miili ya watu 10 tu kati ya 50 waliokuweko kwenye boti hiyo iliyozama katika Ziwa Kivu katika eneo la Idjwi ndiyo imeweza kuopolewa, huku maiti zingine zikipotelea majini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live