Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 11 wamefariki, wengine 4 watoweka ajali ya boti Rwanda

Rwanda Ajaliiiii.jpeg Watu 11 wamefariki, wengine 4 watoweka ajali ya boti Rwanda

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 11 wamethibitishwa kufariki na wengine wanne hawajulikani walipo baada ya mashua kupinduka kwenye mto mashariki mwa Rwanda, afisa mmoja ametangaza Jumamosi.

Ajali hiyo ilitokea Ijumaa jioni kwenye Mto Mugesera wilayani Rwamagana. Boti hiyo ilikuwa imebeba abiria, hasa wakulima waliokuwa wakitoka kuvuna mazao yao katika eneo la Rukumberi wilayani Ngoma, wakielekea wilayani Rwamagana. Boti hiyo ilipinduka kutokana na upepo mkali ulioizamisha

Meya wa wilaya Radjab Mbonyumuvunyi aliwaambia waandishi wa habar kwamba boti hiyo ilikuwa na abiria 46 na kufikia Jumamosi asubuhi, miili 11 ilipatikana, huku watu 31 wakiokolewa,"

"Jitihada zawa kuwatafuta watu wengine wanne bado zinaendelea," alisema Mbonyumuvunyi, akihusisha ajali hiyo na kubeba mizigo kupita kiasi.

Ajali za boti hutokea mara kwa mara katika nchi za eneo la Maziwa Makuu. Mwezi Oktoba mwaka jana takriban watu 30 walikufa maji baada ya mashua kupinduka kwenye mto Congo kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ajali za boti hutokea mara kwa mara kutokana na kupakia abiria na mizigo kupita kiasi, ukosefu wa matengenezo na kusafiri usiku. Abiria wengi pia hawavai maboya ya usalama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live