Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 11 wafariki dunia katika mgodi wa madini Afrika Kusini

Watu 11 Wafariki Dunia Katika Mgodi Wa Madini Afrika Kusini Watu 11 wafariki dunia katika mgodi wa madini Afrika Kusini

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Watu 11 wameuawa mgodi wa madini ya platinam nchini Afrika Kusini, kulingana na kampuni ya uchimbaji madini ya Implats.

Ajali hiyo ilitokea Jumatatu mchana katika eneo la Impala Rustenburg katika jimbo la Kaskazini Magharibi.

Msemaji wa kampuni aliiambia idhaa ya kidijitali ya Afrika Kusini eNCA kwamba watu 88 "walihusika katika tukio hilo" na kwamba watu 11 "kwa bahati mbaya wamefariki dunia kutokana na majeraha".

Operesheni ya uokoaji ndani ya mgodi imekamilika, msemaji huyo aliongeza.

Taarifa ya kampuni ilisema tukio hilo lilihusisha kamba iliyounganishwa na "usafirishaji wa wafanyikazi", ambayo huwapandisha watu juu na ndani ya mgodi. Usafirishaji unajumuisha ngazi tatu, kila moja ikiwa na uwezo wa kubeba watu 35, Implats ilisema.

Chanzo: Bbc