Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 11 wafariki 4 wapofuka baada ya kunywa pombe ya ndizi

0fgjhs19hlicnitq7g Watu 11 wafariki 4 wapofuka baada ya kunywa pombe ya ndizi

Thu, 6 Jan 2022 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Watu hao walianza kupoteza maisha yao tangu Krismasi huku wengine wanne wakipokea matibabu hospitalini baada ya kupofuka Watu watano walikamatwa siku ya Jumatatu, Januari 3, kuhusiana na tukio hilo, akiwemo mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe hiyo Kufuatia kisa hicho, kampeni ya nchi nzima imezinduliwa ili kubana pombe za kienyeji ambazo hazijaidhinishwaWatu 11 wamepoteza maisha yao nchini Rwanda baada ya kunywa pombe ya kienyeji iliyotengenezwa kutumia ndizi.

Inaripotiwa kwamba watu hao walianza kupoteza maisha yao tangu Krismasi huku wengine wanne wakipokea matibabu hospitalini baada ya kupoteza uwezo wa kuona.

Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi nchini Rwanda, watu watano walikamatwa siku ya Jumatatu, Januari 3, kuhusiana na tukio hilo, akiwemo mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe hiyo.

Kulingana na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Rwanda, viwango vya juu vya methanoli vilivyopatikana katika moja ya bia hiyo kwa jina Umuneza, vinaweza kuhusishwa na vifo hivyo.

Kufuatia kisa hicho, kampeni ya nchi nzima imezinduliwa ili kubana pombe za kienyeji ambazo hazijaidhinishwa.

Watu sita wapofuka na kufariki baada ya kunywa pombe haramuKwingineko humu nchini, watu sita kutoka Kijiji cha Jawadho, Njoro, Kaunti ya Nakuru wamepoteza maisha yao baada ya kubugia pombe haramu inayokisiwa kuwa na sumu.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, wahasiriwa walipoteza uwezo wa kuona kabla ya kuangamia kutokana na athari za pombe hiyo.

“Kakangu alienda kupiga mvinyo Jumamosi na aliporejea alianza kulalamikia maumivu makali ya tumbo. Hakuwa na uwezo wa kusema mengi, ila kulalamikia maumivu ya tumbo,” jamaa wa mmoja wa waliofariki aliiambia runinga ya Citizen.

Kufuatia kisa hicho, wakaazi wameizitaka asasi husika kufanya msako katika maeneo yanayouzia vijana pombe haramu.

Wakati huo huo mnamo Agosti 2021, serikali ilimsimamisha kazi OCPD mjini Nakuru na maafisa wengine saba kufuatia vifo vya wakaazi kumi waliobugia pombe haramu.

Mratibu wa Bonde la Ufa George Natembeya alisema kuwa hatua hiyo ilinuia kukabili uuzaji wa pombe haramu kaunti ya Nakuru.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke