Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 100 watekwa kabla ya uchaguzi

95521 C Watu 100 watekwa kabla ya uchaguzi

Fri, 14 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Yaoundé, Cameroon. Wapiganaji nchini Cameroon kutoka maeneo yanayozungumza Kiingereza, waliwateka watu 100 na kuchoma mali katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa wiki iliyopita, shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema leo. Vikosi vya usalama vya serikali pia vilikiuka sheria katika mikoa miwili yenye vurugu,shirika hilo lilisema. "Viongozi awanaotaka eneo hilo lijitenge wanatakiwa watoa maelekezo kwa wapiganaji wao kuacha uhalifu huo dhidi ya raia," mkurugenzi wa Afrika wa HRW, Lewis Mudge alisema katika taarifa ya shirika hilo. "Serikali ya Cameroon inatakiwa kuhakikisha vikosi vya usalama vinaweka kipaumbele kwa raia, kwa kuacha ukiukaji wa sheria, kuweka mbele uwajibishaji wa wahusika." Uchaguzi huo uliofanyika nchi nzima Jumapili unalenga kuchagua bunge jipya na mabaraza ya madiwani. Upigaji kura ulitakiwa ufanyike mwaka 2017 lakini uliahirishwa mara mbili. Lakini ulifunikwa na uasi wa zaidi ya miaka miwili wa jeshi katika Mkoa wa Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi, ambako raia wengi wanaozungumza Kiingereza wanaishi. HRW ilisema vikosi hivyo vilishambulia watu waliokuwa wakitaka kushiriki uchaguzi kama wapigakura au wafanya kampeni, wafanyakazi wa serikali au wagombea. "Waliolengwa ni pamoja na wanachama na wafuasi wa chama cha Social Democratic Front (SDF), ambao wapiganaji hao wanawatuhumu kushindwa kuonyesha mshikamano katika mapambano yao," taarifa hiyo ilisema. Pia walichoma ofisi kadhaa za uchaguzi, ofisi ya posta ambako vifaa vya uchaguzi vilihifadhiwa na angalau nyumba saba za viongozi wa serikali na wagombea. "Badala ya kulinda raia wasivamiwe, vikosi vya serikali navyo vikafanya makosa zaidi dhidi yao," imesema HRW.  

Chanzo: mwananchi.co.tz