Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 10 wapoteza maisha kwenye hujuma za RSF Khartoum, Sudan

Sudan : Watoto Zaidi Ya 1,200 Wamefariki Dunia Tangu Mwezi Mei Watu 10 wapoteza maisha kwenye hujuma za RSF Khartoum, Sudan

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa akali watu 10 wameuwawa Sudan kufuatia hujuma za makombora yaliyofyeauliwa na Kikosi cha Usaidi wa Haraka RSF ambayo yalianguka kwenye msikiti mmoja na majengo mengine kadhaa ya makaazi mjini Khartoum.

Huo ni mkasa wa hivi karibuni kabisa uliosababisha vifo vya raia mjini Khartoum tangu kuzuka kwa mapigano kati ya vikosi tiifu wa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo Abdel Fattah al-Burhan na msaidizi wake wa zamani anayeongoza kikosi cha RSF Mohamed Hamdan Daglo.

Moja ya makundi yaliyokuwa yakiipinga serikali limesema mbali ya watu 10 waliopoteza maisha, wengine 11 wamejeruhiwa kwenye mashambulizi hayo ya RSF yaliyokilenga kitongoji cha Al-Samrab.

Taarifa ya kamati hiyo imefafanua kwamba baadhi ya makombora yalianguka kwenye msikiti, kituo cha afya na maakazi ya watu.

Mapigano ya utumiaji silaha nchini Sudan yalianza Aprili 15 kati ya vikosi vya jeshi na vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwa lengo la kuwania madaraka, na usuluhishi wa kimataifa uliofanywa kwa madhumuni ya kuhitimisha mapigano hayo na kuzikutanisha pande mbili kwenye meza ya mazungumzo haujazaa matunda hadi sasa.

Tofauti kati ya Abdul Fattah al-Burhan, mkuu wa baraza tawala na kamanda wa jeshi la Sudan, na Mohamed Hamdan Dagalo, kamanda wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka, zilidhihirika baada ya kusainiwa kile kilichojulikana kama "makubaliano ya mwongozo" ya kuunda serikali ya kipindi cha mpito na kukabidhi madaraka kwa raia.

Baada ya wito uliotolewa na jeshi wa kuchanganywa vikosi vya RSF kwenye vikosi vya ulinzi, Dagalo alilituhumu jeshi la Sudan kuwa linapanga kubaki madarakani na si kukabidhi madaraka kwa raia, huku jeshi nalo likisema harakati za Vikosi vya Usaidizi wa haraka ni uasi dhidi ya serikali ya mpito.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live