Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 1,412 Zaidi Waambukizwa COVID-19

Bea4332e45b2dc18 Watu 1,412 Zaidi Waambukizwa COVID-19

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 Kenya imefika 134,058

- Wakenya ni 1,324, 88 ni raia wa kigeni huku 771 kati ya walioambukizwa wakiwa wanaume nao 641 ni wanawake

- Katibu Mwangangi alishikilia kwamba Wakenya watazidi kupokea chanjo hiyo bila malipo

- Alithibitisha kuwa wahudumu wa Afya 67, 605 na wale wanaohudumu katika kitengo cha usalama 11, 500 hadi sasa wamepokea chanjo katika awamu ya kwanza

Katibu katika Wizara ya Afya Mercy Mwangangi Jumatano, Machi 31, alitangaza kuwa watu 1,412 wamepata Covid-19, kati ya sampuli ya 9,219 zilizopimwa katika 24 zilizopita.

Kulingana naye asilimia ya maambukizi nchini Kenya sasa imegonga 15.3 ambapo idadi ya walionasa virusi vya corona imefika 134,058.

Kati ya visa hivyo, Wakenya ni 1,324, 88 ni raia wa kigeni huku 771 kati ya walioambukizwa wakiwa wanaume nao 641 ni wanawake.

Wizara hiyo ilisema pia kwamba mgonjwa mwenye umri wa chini zaidia alikuwa mtoto wa miezi 8 naye amkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 94.

Wakati uo huo, Mwangangi alitangaza kuwa wagonjwa 6 waliangamizwa na maradhi hayo hatari katika saa 24 zilizopita ambapo sasa idadi ya wlaiofariki dunia imefika 2,153.

Aidha wagonjwa 389 wamepona ugonjwa huo katika masaa 24 zilizopita.

230 kati hao walikuwa wakihudumiwa makwao nao 159 walikuwa wakiuguzwa katika vituo mbalimmbali vya afya nchini. Jumla ya waliopata nafuu sasa ni 92,679.

Kaunti ya Nairobi bado inaongoza kwa idadi ya maambukizi ikifuatiwa na Mombasa, Kiambu na Kajiado.

Alipoulizwa kuhusu chanjo inayoendelea kote nchini, Katibu huyo alishikilia kwamba Wakenya watazidi kupokea chanjo hiyo bila malipo.

"Chanjo ya AstraZeneca inatolewa bure katika vituo vya afya na hii inajumuisha vituo vya kibinafsi pia," alisisitiza Mwangangi.

Mwangangi alithibitisha kuwa wahudumu wa Afya 67, 605 na wale wanaohudumu katika kitengo cha usalama 11, 500 hadi sasa wamepokea chanjo katika awamu ya kwanza.

Wizara hiyo pia ilitoa wito kwa Wakenya ambao hawakuorodheshwa katika wale ambao walipaswa kupokea chanjo hiyo katika awamu ya kwanza kusubiri hadi zamu yao itakapofika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke