Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto weye rasta ruksa shuleni

Rasta Me Watoto weye rasta ruksa shuleni

Tue, 9 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama kuu nchini Malawi imeamuru mamlaka za elimu nchini humo kuwapokea wanafunzi wenye kufuga rasta katika shule za umma kote nchini.

Mahakama hiyo, iliyoko mashariki mwa jiji la Zomba, ilikuwa ikitoa uamuzi juu ya ombi lililowasilishwa na watoto wawili wenye imani ya kirasta (Rastafarian) ambao walikataliwa kujiunga na shule za umma mwaka wa 2016 na 2010.

Wanafunzi hao wawili, hata hivyo, wamekuwa wakihudhuria shule baada ya kupata zuio la mahakama. Mazungumzo kati ya Jumuiya ya Rastafarian nchini Malawi na mwanasheria mkuu wa nchi hiyo kutatua suala hilo yamegonga mwamba na kusababisha kesi ya kisheria ya muda mrefu, ambayo uamuzi wake ulitolewa Jumatatu.

Jaji Zione Ntaba alisema kuwazuia watoto wenye rasta ama dreadlocks kwenda shule ni kuvunja na kuwanyima haki yao ya kupata elimu.

"Wizara ya Elimu inapaswa kutoa tamko la kuruhusu watoto wote wa jamii ya Rastafarini wenye rasta waruhusiwe darasani. Waraka unapaswa kutolewa ifikapo tarehe 30 Juni," Jaji Ntaba aliamuru.

Kesi hiyo iliwasilishwa na mashirika matatu ya kutetea haki za binadamu kwa niaba ya jamii ya watu wenye imani ya Rastafarian nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live