Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto watano wafariki Afrika Kusini baada ya basi ya shule kugongana na treni

Watoto Watano Wafariki Afrika Kusini Baada Ya Basi Ya Shule Kugongana Na Treni.png Watoto watano wafariki Afrika Kusini baada ya basi ya shule kugongana na treni

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: Voa

Watoto watano walifariki Jumatano baada ya treni kugongana na basi la shule nchini Afrika Kusini, na kujeruhi wengine 20, wizara ya uchukuzi ilisema katika taarifa.

Ajali hiyo ilitokea nyakati za alasiri karibu na kijiji cha Mafube, karibu na mji wa Middelburg, umbali wa kilomita 180 kaskazini mashariki mwa Johannesburg, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Serikali ilithibitisha katika taarifa “ Ajali mbaya kwenye njia ya kivuko, ilihusisha basi na treni. Ilisababisha vifo vya watoto watano na wengine 20 kujeruhiwa.”

Naibu waziri wa uchukuzi Mkhuleto Hlengwa alisema “ Usalama wa watoto wetu ni muhimu na ni jambo la kushtusha kushuhudia maafa hayo.”

Polisi waliripoti kwamba dereva wa basi hiyo alitoroka eneo la tukio baada ya ajali hiyo, wizara ya uchukuzi ilisema.

Chanzo: Voa