Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto waokolewa huku polisi wa Zimbabwe wakifukua makaburi ya siri

Watoto Waokolewa Huku Polisi Wa Zimbabwe Wakifukua Makaburi Ya Siri Watoto waokolewa huku polisi wa Zimbabwe wakifukua makaburi ya siri

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Polisi nchini Zimbabwe wanasema wamemkamata mshukiwa na kiongozi wa madhehebu ya kidini katika kijiji kimoja kaskazini mwa jimbo la Mashonaland Magharibi na kuokoa makumi ya wanawake na watoto.

Ishmael Chokurongerwa, 56, ambaye anaongoza madhehebu ya Gore Jena Penyeranyika alikamatwa pamoja na washiriki wengine saba siku ya Jumanne, msemaji wa polisi Paul Nyathi alisema katika taarifa.

Polisi walisema wengi wa watoto 251 waliopatikana katika shamba la Bw Chokurongerwa huko Nyabira, yapata kilomita 34 (maili 21) kaskazini-magharibi mwa mji mkuu, Harare, hawakuwa na vyeti vya kuzaliwa na hawakuruhusiwa kuhudhuria shule.

Polisi pia waligundua kaburi katika shamba hilo ambapo watu 16 wamezikwa kwa siri, wakiwemo watoto wachanga saba ambao mazishi yao hayakusajiliwa na mamlaka.

Watoto waliookolewa "walikuwa wakitumiwa kufanya shughuli mbalimbali za kimwili kwa manufaa ya uongozi wa kikundi", taarifa ya polisi ilisema.

"Polisi pia walibaini kuwa watoto wote walinyanyaswa kama vile kazi za bei nafuu, wakifanya kazi za mikono kwa jina la kufundishwa masomo ya maisha," iliongeza.

Bw Chokurongerwa, ambaye anajiita "Nabii Ishmael", aliwaambia waandishi wa habari kuwa "hajui haki za wanawake na watoto".

Mmoja wa washirika aliwaambia waandishi wa habari kwamba elimu rasmi shuleni haitakiwi na Mungu “kwa sababu yale ambayo watoto wanafundishwa huko ni kinyume na mafundisho ya Mungu”.

Chanzo: Bbc