Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wanne wauawa katika shambulio dhidi ya lori la mafuta mashariki mwa DRC

Watoto Wanne Wauawa Katika Shambulio Dhidi Ya Lori La Mafuta Mashariki Mwa DRC.png Watoto wanne wauawa katika shambulio dhidi ya lori la mafuta mashariki mwa DRC

Fri, 16 Aug 2024 Chanzo: Voa

Watu 7 wakiwemo watoto wanne walifariki mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya watu wenye silaha kushambulia lori la mafuta, vyanzo vya eneo hilo viliiambia AFP Alhamisi.

Lori hilo “lilichomwa moto na watu wenye silaha wasiojulikana Jumatano ”, karibu na mji wa Katwiguru katika jimbo la Kivu Kaskazini, Jerome Nyamuhanzi, kiongozi wa kundi la vijiji katika wilaya ya Rutshuru ambako shambulio hilo lilifanyika, aliiambia AFP.

Nyamuhanzi alisema, baada ya shambulio, “bomu lililokuwa ardhini liliokotwa na watoto hao wakidhani ni kitu cha kuchezea na kifaa hicho kililipuka,” na kuongeza kuwa “watoto wanne walifariki papo hapo”.

Vyanzo viwili vya hospitali viliiambia AFP kwamba watu sita walijeruhiwa pia katika shambulio hilo, vikisema liliuua jumla ya watu 7, wakiwemo watoto wanne.

Haikufamika wazi nani alihusika na shambulio hilo, katika eneo ambalo limekumbwa na machafuko kwa miaka kadhaa.

Chanzo: Voa