Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wanarubuniwa kuingia kwenye mapenzi ya jinsia moja- Askofu Uganda

Watoto Wanarubuniwa Kuingia Kwenye Mapenzi Ya Jinsia Moja  Askofu Uganda Watoto wanarubuniwa kuingia kwenye mapenzi ya jinsia moja- Askofu Uganda

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: bbc

Askofu Mkuu wa Kanisa la Uganda Stephen Kaziimba Mugalu ameiomba serikali kuweka utaratibu wa wanafunzi kuwaripoti watu wanaowarubuni kuingia katika mapenzi ya jinsia moja.

Askofu Kaziimba amesema kuwa kama kiongozi wa Kanisa, amepokea taarifa za watu wakiwa katika zoezi la kuwaingiza watoto wa shule katika vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Akitoa ujumbe wake wa Krismasi kwenye kanisa la Namirembe, Kampala, siku ya Jumanne, Askofu Mkuu aliwaonya wazazi, walimu na wanafunzi dhidi ya watu wanaowavutia katika vitendo viovu.

“Ninataka kuwatahadharisha wanafunzi wote, wazazi, na walimu kwamba kuna watu wabaya wanaojaribu kuwavutia watoto katika mapenzi ya jinsia moja kwa kuwaahidi pesa na ufadhili.

Naiomba Serikali iweke utaratibu rahisi ambao watoto wanaweza kutoa taarifa za watu hawa kwa mamlaka zinazohusika ambazo zinaweza kuchunguza na kuchukua hatua stahiki,” alisema.

“Kwa wale wanaoingiza watoto katika mapenzi ya jinsia moja, nataka kutoa onyo kali kwenu. Haya si maneno yangu, bali ni maneno ya Yesu: ‘Yeyote atakayemkosea mmojawapo wa wadogo hawa… ili kujikwaa, ingekuwa afadhali wafungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni na kuzamishwa katika kilindi cha bahari,” aliongeza.

Askofu Kaziimba alikaririwa akisema kuwa kanisa analoliongoza daima litazingatia mafundisho ya Biblia kwamba ndoa ni kati ya mwanaume mmoja na mwanamke mmoja.

Kwa upande wa serikali mtandao wa Monitor umeandika kuwa mwenyekiti wa Maadili na Uadilifu, Dk Annette Kezaabu, alithibitisha wasiwasi wa kasisi huyo. “Nimekusanya ushahidi mwingi, taarifa nyingi kuhusu jinsi watoto hawa walivyosikia kuhusu mapenzi ya jinsia moja, wanachofikiria kuhusu hilo na mambo mapya waliyojifunza kuhusu hilo; wengine hujifunza kutoka kwa marafiki, wengine kutoka Tiktok lakini inapokuwa karibu na nyumbani, inaonekana ni mtindo mpya wa maisha ya sasa, "alisema.

Chanzo: bbc