Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wafariki kwa kunywa sumu

Sumu Pc Data.jpeg Watoto wafariki kwa kunywa sumu

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto watatu wa familia moja wenye umri wa miaka 6, 13 na 16 Nchini Afrika Kusini wamefariki dunia baada ya kunywa kinywaji kinachodaiwa walipewa na baba yao.

Kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Polisi katika jimbo la Gauteng nchini humo zimesema mpaka sasa haijafahamika kama kinywaji hicho kilikuwa na sumu, lakini taarifa za awali zinaeleza kuwa baba wa watoto hao naye alijaribu kujiua jambo linaloonyesha alikuwa na nia ovu.

Habari zaidi kutoka nchini Afrika kusini zinaeleza kuwa watoto hao  walifariki dunia wakiwa shuleni  na mmoja akiwa njiani kupelekwa hospitalini na inadaiwa kwamba mtoto mwingine wa familia hiyo ambaye naye alikunywa kinywaji hicho hali yake ni mbaya.

Familia hiyo iliyokuwa na jumla ya watoto watano, mtoto mmoja pekee kati ya hao ndiye hajadhurika kwa kuwa hakunywa kinyaji hicho.

Kwa mujibu wa taarifa za Vyombo Vya Habari nchini humo bado kuna utata mahali alipo baba wa watoto hao kwa sasa, na taarifa nyingine zinadai kuwa mama wa watoto hao naye amelazwa hospitalini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live