Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wa shule 'warushiwa vitoa machozi' maandamano Kenya

Maandamo Yafanyika Kenya Licha Ya Marufuku Ya Polisi Watoto wa shule 'warushiwa vitoa machozi' maandamano Kenya

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Watoto 53 wa shule wamekimbizwa hospitalini baada ya gesi ya kutoa machozi kuripotiwa kuanguka darasani mwao wakati wa maandamano yanayoendelea.

Daktari Aron Shikuku, mmiliki wa hospitali ya Eagle Nursing Home, ameithibitishia BBC, kwamba watoto hao wamehudumiwa na kwa sasa wako chini ya uangalizi wa kimatibabu.

“Wamekuwa hospitalini kwa takriban saa nne wakitibiwa kwa mshtuko baada ya kuzidiwa na moshi wa mabomu ya machozi. Hakuna majeruhi aliyeripotiwa.”, alisema Dk Shikuku.

Tukio hili lilitokea wakati wa maandamano ya kitaifa ya kupinga kupanda kwa gharama ya maisha, ambayo yamesababisha hasara kubwa.

Visa viwili vya vifo vimeripotiwa huku waandamanaji wakivamia kituo cha polisi na kukichoma moto katika kaunti inayopakana na Mji Mkuu wa Nairobi, na mtu mwingine kupoteza maisha baada ya gari la polisi kuchomwa moto kando ya Barabara ya Nairobi Expressway huko Mlolongo nje kidogo ya jiji la Nairobi.

Kutokana na wasiwasi kuhusu kile alichokiita kuongezeka kwa ghasia kutoka kwa mamlaka, kiongozi wa Upinzani Raila Odinga amesitisha mkutano uliopangwa kufanyika katika uwanja wa Kamukunji viungani mwa jiji la Nairobi..

Kukatizwa kwa usafiri na biashara kunaendelea kuathiri kaunti mbalimbali, huku waandamanaji wakiamua kuwasha moto barabarani na kugoma kujihusisha na shughuli kama vile michezo ya soka kwenye vituo vya mabasi.

Hali bado ni tete na video zinazonasa matukio haya zimesambazwa sana mtandaoni.

Chanzo: Bbc