Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wa Rais kujumuishwa kwenye Ujumbe wa Serikali kwenda Dubai

Hage Geingob Watoto wa Rais kujumuishwa kwenye Ujumbe wa Serikali kwenda Dubai

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya WaNamibia wamekasirishwa baada ya kujua kwamba watoto wanne wa Rais Hage Geingob walijiunga na ujumbe wa serikali kwenye mkutano wa hali ya hewa wa COP28.

Walikuwa miongoni mwa watu sita kutoka familia ya rais iliyoorodheshwa kama sehemu ya ujumbe wa Namibia huko Dubai.

Ofisi ya Rais Geingob ilithibitisha siku ya Jumatatu kwamba watoto wake walifika katika jiji hilo, lakini ilikana madai ya kwamba safari yao ilifadhiliwa na serikali, pia ofisi hiyo haikusema wanafamilia wengine gharama zao zililipwa na nani.

"Rais Geingob na Bibi Geingos(Mkewe) walilipia ndege na gharama za malazi za watoto wao," Rais wa Namibia alipost X siku ya Jumatatu.

"Wanamibia na vyombo vya habari vinapaswa kuondoa mashaka kwamba hakuna hata senti moja ya fedha za umma zimetumika kwa watoto wa Rais."

Rais aliongeza kwamba madai hayo yalikuwa "yenye na yamechochewa kisiasa" na yanalenga kuvuruga "kazi nzuri" ya Rais Geingob na ujumbe wa Namibia huko COP28.

Lakini baadhi ya WaNamibia wamepuuzia mbali jibu la rais kama lisilotosheleza, wakisema haliwezi kuthibitisha kwamba safari ya watoto wa Rais Geingob na wanafamilia wake ilifadhiliwa kwa kibinafsi.

Baadhi ya wakosoaji pia wameitaka ofisi ya rais kueleza jukumu la wanafamilia wake kwenye Mkutano wa COP28 na kwa nini waliorodheshwa kwenye ujumbe wa serikali ikiwa safari yao ililipwa kibinafsi.

"Mnaamini sisi ni wapumbavu? Kwanini wangeweza kuorodheshwa kwenye orodha ya wajumbe kama hawako sehemu yake? Kuna umuhimu gani wa kuwepo kwao Dubai pamoja na wajumbe wa serikali?" mmoja wa WaNamibia alijibu X.

"Tunatarajia ripoti kamili itakayowasilishwa [bungeni]," alisema Mbunge wa Namibia Inna Hengari.

Awali, alikuwa ameikosoa serikali kwa kuripotiwa kufadhili safari ya familia ya rais, huku wakidai hawana fedha za kufanikisha safari ya mbunge na afisa wa bunge kwenda COP28.

Ghadhabu hiyo inaonyesha upinzani mkubwa dhidi ya serikali za Kiafrika kwa kutuma ujumbe mkubwa kwenye COP28, ambao baadhi ya wananchi wanasema unadhihirisha ubadhirifu wa fedha.

Baadhi ya serikali, ikiwemo Nigeria, Tanzania, na Kenya, zimejitetea kwa kusema kuwa wajumbe wengi hawalipwi na serikali kwa kuwa wanawakilisha vyombo vya habari, asasi za kiraia, na taasisi binafsi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live